1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Jeshi la Ukraine latangaza mafanikio katika uwanja wa vita

8 Oktoba 2023

Na katika uwanja wa mapambano huko nchini Ukraine, Jeshi la Ukraine linasema linaendelea kuvishambulia vikosi vya Urusi kwenye sehemu mbili muhimu upande wa mashariki na kusini hatua ambayo imetoa mafanikio ya kadri.

https://p.dw.com/p/4XG3V
Ukraine | Gepard-Panzer in der Region Kiew
Picha: Sergei Supinsky/AFP/Getty Images

Taarifa ya jeshi hilo imelitaja eneo la kusini mwa mji wa Bakhmut, karibu na  kijiji cha Andriyivka, kuwa kumekuwa na mafanikio ya kiasi. Wakati mji huo ukiwa bado katika udhibiti wa Urusi, jeshi la Ukraine limefanikiwa kuidhibiti reli muhimu ya kimkakati.Katika uwanja wa mapambano kusini katika mkoa wa Zaporizhzhya, kuna kile Ukraine ilichokiita "mafanikio ya kiasi" yaliyopatikana kaskazini mwa vijiji vya Kopani na Novoprokopivka Kimsingi katika ukanda huo, jeshi la Ukraine limekuwa likikabiliana na ngome imara ya Urusi.