Maandamano ya upinzani ya kupinga mapinduzi ya kijeshi nchini Myanmar yamefanyika, yakijumisha jamii ya makabila madogo, waandishi, washairi na wafanyakazi wa sekta ya usafiri miongoni mwa waliojitokeza katika kushinikiza kufikisha kikomo utawala wa kijeshi pamoja na kuachiwa huru mwanasiasa Aung San Suu Kyi na wengine.