Waziri wa Mambo ya Nje ya Israel, Gabi Ashkenazi amewasili mjini Cairo kwa ajili ya mazungumzo na maafisa waandamizi wa Misri, yenye lengo la kuunga mkono hatua ya kusitisha mapigano, iliyoridhiwa na Israel kwa upande mmoja na wapiganaji wa Hamas wenye kulitawala eneo la Ukanda wa Gaza.