1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

50 plus One inastahili kuondolewa Ujerumani

30 Julai 2018

Afisa Mkuu Mtendaji wa Bayern Munich Karl Heinz Rummenigge ameutaka uongozi wa Ligi Kuu ya Ujerumani Bundesliga kuondoa sheria inayowazuia wawekezaji kununua vilabu vya soka Ujerumani.

https://p.dw.com/p/32KfP
Karl-Heinz Rummenigge
Picha: picture alliance / Matthias Balk/dpa

Sheria hiyo inajulikana kama 50 plus One. Sheria hiyo inawazuia wawekezaji kuwa na zaidi ya asilimia 49 ya hisa katika klabu. Rummenigge anasema ili vilabu vya Ujerumani kusonga mbele katika mashindano ya Ulaya ni sharti sheria hiyo iondolewe ndiposa vilabu viweze kuwavutia wachezaji wenye hadhi ya juu.

Mwandishi: Jacob Safari

Mhariri: Yusuf Saumu