1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ABIDJAN: Serikali ya Ivory Coast na Waasi wakutana Afrika Kusini.

25 Machi 2005
https://p.dw.com/p/CFTe

Rais Laurent Gbagbo wa Ivory Coast atakutana na rais Thabo Mbeki wa Afrika Kusini ili kufanya mazungumzo ya amani ya Ivory Coast.

Rais Mbeki alichaguliwa na Umoja wa nchi za Afrika kusuluhisha mzozo wa Ivory Coast ambayo iligawanyika baada ya kushindwa jaribio la kuipindua serikali ya rais Gbagbo September mwaka 2002.

Rais Mbeki amezialika pande zote mbili serikali na upinzani mjini Pretoria katika mkutano wa kutafuta suluhisho baina ya pande hizo mbili.

Upande wa upinzani umekubali mualiko huo na rais Gbagbo ataandamana na waziri wake mkuu Seydou Diarra.