Afrika Kusini kuzifunga kambi za wakimbizi
15 Agosti 2008Mahakama ya katiba ya Afrika Kusini imekuwa ikisikiliza ombi lililowasilishwa na kundi linalowatetea wakimbizi kuitaka ibatilishe uamuzi wa mahakama kuiruhusu serikali izivunje kambi za wakimbizi. Wanaharakati hao wanaitaka serikali iziache kambi hizo mpaka mkakati kamili wa kuwajumulisha wakimbizi katika jamii, wengi wao wakiwa waafika, utakapotayarishwa.
Leo ilikuwa siku ya mwisho iliyotolewa na serikali ya jimbo la Gauteng kufungwa kwa kambi sita ambako ni makaazi ya watu 2,500. Wakimbizi katika jimbo la Western Cape, ambako mji wa Cape Town unapatikana, wana majuma kadhaa kupanga hatua za kuchukua huku maafisa wa serikali ya mkoa huo wakipania kubomoa makaazi zaidiy a 40 ifikapo tarehe 3 mwezi ujao.
Kambi hizo zilianzishwa mwezi Juni kuwahifadhi wahanga wa machafuko yaliyodumu muda wa majuma mawili katika vitongoji duni yaliyosababisha vifo vya watu 62 na mamia ya wengine kujeruhiwa. Mamia ya maelfu ya wengine walilazimika kukimbia kuyaokoa maisha yao.
Mwanzoni mwa operesheni hiyo kulikuwa na mashirika na taasisi za serikali zilizokuwa zikitoa misaada hata wakati watu walipkuwa bado katika vituo vya polisi na makanisani kabla kambi za usalama kuanzishwa. Shirika la msalaba mwekundu lilitoa chakula, mablanketi nausharui kwa watu kwenda kutafuta huduma za afya na matibabu kwa kuwa baadhi yao walijeruhiwa wakati waliposhambuliwa nje ya makaazi yao.
Wakati kambi zilipojengwa shirika la msalaba mwekundu lilifanya kazi katika baadhi ya kabi hizo kwa kuwa halingeweza kuzifikia kambo zote. Kambi sita kambi kumi zilishungulikiwa na kama zilikuwa 20 basi sehemu ya hizo pekee ziliweza kufikiwa.
Juhudi ya kuwasaidia wakimbizi ilipoanza, shirika la msalaba mwekundu liliwahudumia watu takriban elfu 33. Kufikia mwezi Juni mwaka huu idadi hiyo ilipungua kufikia takriban watu elfu 20 na wakati huu katika maeneo yanyolengwa kuwahamisha wakimbizi, wakimbizi yapata 4,000 wamekuwa wakihudumiwa.
Mwenyekiti wa shirika la msalaba mwekundu tawi la Afrika Kusini, Bi Mandisa Kalako Williams, anaeleza kwa nini idadi hii imepungua.
´´Hii ni kwa sababu kadri siku zilivyopita, wakimbizi wengine waliondoka makambini. Wengine walirudi katika jamii zao ambako walijihisi wako salama na wengine wakarejea nchini mwao. Kwa hiyo idadi iilipungua.´´
Shirika la msalaba mwekundi nchini Afrika Kusini limesema hatua yoyote ya kuwahamisha wakimbizi ni jukumu la serikali. Bi Mandisa amesema shirika hilo lina mamlaka tu ya kutoa misaada ya kibinadamu na liko tayari kuingilia kati wakati wowote ule kuwasaidia wakimbizi.
Wakati kambi zitakapofungwa wakimbizi watatolewa kwenye kambi hizo na pengine kurudishwa katika nchi walizotokea. Je shirika la msalaba mwekundu litafanya nini katika hali hii? Bi Mandisa anaeleza.
´´Tunaweza kusaidia kwa sababu tunazo fedha na raslimali zilizotolewa kuwasaidia wakimbizi hawa wakati wakiwa makambini. Tunaweza kutumia raslimali hizo kuhakikisha kuwa usafiri wao unafanyika vizuri, wana chakula cha kutosha katika safari na tunaweza kuwaunganisha na mashirika ya kitaifa ya nchi wanakorejea.´´
Jambo lengine linaloweza kutokea ni iwapo wakimbizi wataondolewa makambini na kuhamishwa katika sehemu nyingine nchini. Bi Mandisa Kalako wWilliams anasema shirika la msalaba mwekundu nchini Afrika Kusini linatakiwa liw tayari kusaidia ili kuhamishwa kwa wakimbizi hao kusiwaletee matatizo mengine.
´´Je wana mahitaji msingi nyumbani? Sabuni, chakula na mablanketi? Pengine watakuwa bado wanayo mablanketi waliyopewa lakini tunataka kuhakikisha popte wanakokwenda maisha yao hayakabiliwi na matatizo mengi ambayo tayari yamewakuta´´
Shirika la msalaba mwekundu linazungumzai kuwajumuisha wakimbizi katika jamii. Bi Mandisa anasema watashirikiana na jamii zitakazowapokea wakimbizi hao katika miradi ya maendeleo na kuhakikisha wanaishi katika hali nzuri. Hata hivyo Bi Mandisa amekiri kwamba kuna changamoto. Amesema ni vigumu kwa shirika la msalaba mwekundu kugawa chakula kwa nyumba moja na nyumba jirani ikiwa na watu wanaotesa kwa njaa.
Hata hivyo amesisitza kwamb aili kuwepo uwiano, ipo haja ya kuijumuisha jamii inayowapokea wakimbizi ili ijihisiina umuhimu kwa shirika la msalaba mwekundu.