Nchini Afrika Kusini raia wanapiga kura kuwachagua viongozi wa serikali za mitaa. Katika kujua hali iliovyo kuhusiana na uchaguzi huo DW imezungumza na mwandishi habari Bryson Bichwa aliyeko Pretoria, Afrika Kusini na kwanza anatupa taswira ya yaliyojiri tangu vituo vya upigaji kura vilipofunguliwa.