1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

AFRIKA: Ripoti ya shirika la afya yaonyesha kuongezeka kwa TB Afrika.

25 Machi 2005
https://p.dw.com/p/CFTl

Shirika la Afya duniani limetangaza kuongezeka kwa ugunjwa wa kifua kikuu katika bara la Afrika.

Taarifa iliyotolewa na shirika hilo imesema kuwa maambukizo ya ugonjwa wa ukimwi yanafanya ugonjwa wa Kifua kikuu kuongezeka kwa haraka.

Katika mwaka wa 2003 watu milioni tisa waliambukizwa ugonjwa wa kifua kikuu duniani huku watu millioni mbili kati ya hao wakitoka bara la Afrika.