Wiki hii Rais Samia wa Tanzania akutana na viongozi wa vyama 19 vya siasa vilivyosajiliwa katika taifa hilo. Na nchini Kongo chama cha rais wa zamani Kabila PPRD na muungano wa FCC wasusia zoezi la uandikishaji wapiga kura katika mikoa 10. Na huko Kenya Rais William Ruto kwa mara ya kwanza tangu alipoingia madarakani azungumza na waandishi habari na kusema Kenya haitoshindwa kulipa madeni yake.