Afya na jamii
10 Mei 2012Mpango wa uzazi ni mada muhimu katika mfululizo wa vipindi vya Noa Bongo, kwani mada hii inagusia maadili ya jamii na maisha kwa jumla, njia za mpango wa uzazi na pia masuala ya kijinsia - hasa kuhusu mabadiliko ya kimawazo katika muda wa miongo ya hivi karibuni barani Afrika. Na Noa bongo pia inatambua juhudi za kutupilia mbali baadhi ya imani na tamaduni katika kupambana na magonjwa kama vile Ukimwi.
Mkazo ulitolewa katika kuimarisha juhudi za kibinafsi kukabiliana na magonjwa na pia kuimarishwa njia za kupata habari muhimu kuhusu masuala ya afya. Juhudi au mabadiliko ya kiwango chochote kile huchangia pakubwa juhudi za kuboresha maisha ya familia na jamii kwa jumla, na ndio sababu vipindi vya Noa Bongo vinalenga kukupa fursa kuwa na mtazamo na kuelekeza juhudi za kila mmoja wetu katika kuboresha afya.