AHMEDABAD. Watu 17 wauwawa katika ajali ya garimoshi nchini India.
21 Aprili 2005Matangazo
Watu wasiopungua 17 wameuwawa katika ajali ya garimoshi magharibi wa India. Garimoshi la abiria liligongana na garimoshi la kubeba mizigo ambalo lilikuwa limesimama, kilomita 30 kutoka wilaya ya Vadodara, magharibi mwa jimbo la Gujarat.
Imeripotiwa kwamba watu zaidi ya 150 wamejuruhiwa na maafisa wanahofu idadi ya vifo huenda ikaongezeka. Mabehewa manne ya garimoshi hilo yaliwacha reli na kuanguka baada ya kugongana na garimoshi lengine.