1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Aina mpya ya vyandarua vya kuzuia mbu

12 Aprili 2018

Wanasayansi wametengeza neti mpya zilizowekwa kemikali ijulikanayo kama Piperonyl butoxide ambayo ni kali na mbu hawawezi kumudu ikilinganishwa na kemikali iliyokuwa ikitumika katika kipindi cha nyuma

https://p.dw.com/p/2vuWB
Simbabwe Moskitozelt
Picha: DW/P. Musvanh

Utafiti mpya umegundua kuwa aina mpya ya vyandarua vya kuzuia mbu vitasaidia katika vita dhidi ya ugonjwa Malaria baada ya kemikali inayotumika katika vyandarua vya zamani kuzoeleka na mbu. Mbu wanaosababisha Malaria wanazoea kwa kasi kemikali inayotumika na hivyo kutengeza kinga mwilini mwao ili wasidhurike na kemikali hiyo hivyo kuvikewa vita dhidi ya Malaria barani Afrika katika hatari.

Wanasayansi wametengeza neti mpya zilizowekwa kemikali ijulikanayo kama Piperonyl butoxide ambayo ni kali na mbu hawawezi kumudu ikilinganishwa na kemikali iliyokuwa ikitumika katika kipindi cha nyuma ya pyrethroid. Utafiti wa miaka miwili uliouhusisha zaidi ya watoto 15,000 nchini Tanzania umegundua kuwa matumizi ya neti hizo mpya umepunguza maambukizi ya Malaria kwa asilimia 44.

Kulingana na takwimu za shirika la afya duniani, WHO, Watu milioni 216 duniani waliugua Malaria mwaka 2016, huku watu 445,000 wakifariki kutokana na ugonjwa huo.