1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ajali ya barabarani yauwa 26, yajeruhi 28 Ivory Coast

7 Desemba 2024

Ajali mbaya ya gari nchini Ivory Coast imepoteza maisha ya watu 26 papo hapo na kuwajeruhi wengine 28, kwa mujibu wa mamlaka za nchi hiyo.

https://p.dw.com/p/4nrf9
Ajali ya barabarani.
Ajali ya barabarani.Picha: AFP

Ajali hiyo ya jana iliyohusisha mabasi mawili katika eneo la magharibi mwa nchi hiyo ilisababisha moto uliowateketeza kabisa watu 10 kati ya 26 waliopoteza maisha yao.

Picha za video zilizorushwa na vyombo vya habari vya huko zinayaonesha magari hayo mawili yakiteketea kwa moto.

Soma zaidi: Côte d'Ivoire yaongeza wanajeshi, ajira kukabiliana na wanamgambo

Ajali za barabarani ni jambo la kawaida katika taifa hilo la Afrika Magharibi kutokana na barabara mbovu na uendeshaji wa ovyo, ambapo kila mwaka watu 1,000 hupoteza maisha yao, kwa mujibu wa wizara ya usafiri nchini humo.

Mwezi uliopita, watu 21 walikufa na wengine 10 kujeruhiwa kwenye ajali kama hizo.