1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JangaAfrika

Ajali ya Boti yaua 38 DRC, zaidi ya 100 hawajulikani walipo

21 Desemba 2024

Watu 38 wamefariki na zaidi ya 100 bado hawajulikani walipo nchini Kongo baada ya kivuko kilichokuwa kimezidisha mzigo kupinduka katika mto Busira.

https://p.dw.com/p/4oTKP
Ajali ya Feri katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo
Ajali za boti zimekuwa ni jambo la kawaida katika mito na maziwa ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, ambako miundombinu ya usafiri bado ni duni sana.Picha: Alain Uaykani/GOMA/Xinhua/picture alliance

Watu thelathini na wanane wamethibitishwa kufariki na zaidi ya 100 bado hawajulikani walipo nchini Kongo baada ya kivuko kilichozidisha mzigo — kilichokuwa kimejaa watu waliokuwa wakirudi nyumbani kwa ajili ya Krismasi — kupinduka katika mto Burisa Ijumaa usiku, kulingana na maafisa wa eneo hilo na mashuhuda.

Watu ishirini wamethibitishwa kuokolewa hadi sasa. 

Kivuko hicho kilikuwa kinasafiri kaskazini-mashariki mwa Kongo kama sehemu ya msafara wa vyombo vingine, na abiria walikuwa hasa wafanyabiashara waliokuwa wakirudi nyumbani kwa ajili ya Krismasi, alisema Joseph Joseph Kangolingoli, meya wa Ingende, mji wa mwisho kabla ya eneo la ajali. 

Kupinduka kwa kivuko hicho kumetokea chini ya siku nne baada ya boti nyingine kupinduka kaskazini-mashariki mwa nchi, na kusababisha vifo vya watu 25. 

Ajali ya boti yauwa zaidi ya watu 50 DR. Kongo

Kwa mujibu wa Ndolo Kaddy, mkazi wa Ingende, kivuko hicho kilikuwa na "zaidi ya watu 400 kwa sababu kilisimama katika bandari mbili, Ingende na Loolo, njiani kuelekea Boende, hivyo kuna sababu ya kuamini kwamba kulikuwa na vifo zaidi." 

Soma pia: Watu wasiopungua 25 wamekufa ajali ya boti DR Kongo

Maafisa wa Kongo mara nyingi wameonya dhidi ya kuzidisha mzigo na kuahidi kuchukua hatua dhidi ya wale wanaokiuka hatua za usalama wa usafiri wa majini. Hata hivyo, katika maeneo ya mbali ambako abiria wengi wanatoka, wengi hawawezi kumudu usafiri wa umma kwa barabara chache zinazopatikana. 

Watu wasiopungua 78 walikufa maji mwezi Oktoba wakati boti iliyozidisha mzigo ilipozama mashariki mwa nchi hiyo, huku watu 80 wakipoteza maisha katika ajali kama hiyo karibu na Kinshasa mwezi Juni.