1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ANC yahitaji kiongozi mwenye maadili-anasema Mbeki

Oummilkheir16 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/CcLM

Polokwane-Afrika Kusini:

Rais Thabo Mbeki wa Afrika kusini,akihutubia mkutano mkuu wa chama cha African National Congress hii leo amesema” ANC inahitaji kiongozi mwenye kufuata maadili,sawa na walivyokua viongozi waliowatangulia”.Matamshi hayo yamelengwa dhidi ya mpinzani wake,makamo wa zamani wa rais Jacob Zuma,anaekabiliwa na hatari ya kufunguliwa mashtaka ya kuhusika na rushwa..Mamia ya wafuasi wa makamo mwenyekiti wa ANC Jacob Zuma walihanikiza kwa nyimbo kujibu hutuba ya mkuu wa chama tawala na rais wa Afrika kusini Thabo Mbeki.Wanachama zaidi ya elfu nne wanaohudhuria mkutano huo mkuu wanatakiwa wamchague mmoja kati ya watetezi hao wawili kukiongoza chama chao cha ANC kwa kipindi cha miaka mitano ijayo.Rais Thabo Mbeki amebakiwa na miaka miwili madarakani na katiba ya Afrika kusini haimruhusu kutetea kwa mara ya tatu wadhifa wa rais.Wajumbe wa ANC wanatazamiwa kumchagua kiongozi wao mpya kesho, siku ya pili ya mkutano mkuu huo wa siku tano katika mji huo wa Polokwane katika jimbo la Limpopo,kaskazini magharibi ya Afrika kusini.