1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ANC yapata rais mpya.

19 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/CdkA

Polokwane.Wajumbe wa chama tawala nchini Afrika kusini , ANC wamemchagua Jacob Zuma kuwa rais mpya wa chama hicho. Amemshinda mpinzani wake na ambaye ni mkuu wa sasa wa chama hicho Thabo Mbeki , ambaye alimfuta kazi Zuma miaka miwili iliyopita wakati akiwa makamu rais wa nchi hiyo baada ya madai ya rushwa yalipojitokeza yakimhusisha Zuma. Ushindi wake unamhakikishia kuwa rais baada ya Mbeki kuondoka madarakani mwaka 2009.

Ushindani baina ya Zuma na Mbeki umesababisha mgawanyiko mkubwa katika mkutano huo mkuu wa chama unaofanyika katika mji wa Polokwane kaskazini mwa nchi hiyo ambao unamalizika kesho Alhamis.