Mtaa wa Korogocho ni moja ya maeneo ya mabanda jijini Nairobi . Katika makala ya Afya Yako, Bernard Maranga anaangazia utupaji wa taka mahala pasipotakiwa unavyoathiri afya za wakazi wa eneo hilo. Wengi wamepatwa na kikohozi, huku magonjwa ya mlipuko kama kipindupindu nayo yakiwa tishio.