AYODHYA Watu watano wauwawa na polisi nchini India
6 Julai 2005Matangazo
Watu watano waliokuwa na bunduki wameuwawa na polisi mjini Ayodhya kazkazini mwa India, baada ya kulivamia eneo la kidini na mtu mwengine wa sita akajilipua kwa bomu. Watu hao wasiojulikana walilivamia jengo ambalo lina hekalu la mfalme Ram.
Hata hivyo jengo hilo linapiganiwa na wahindi na waislamu limekuwa shina la machafuko kati ya makundi hayo mawili. Mwaka wa 1992 makundi ya wahindi waliubomoa msikiti mahala hapo, wakisema ulijengwa mahala hapo ambapo Ram alizaliwa maelfu ya miaka iliyopita.
Hakuna kundi ambalo limedai kufanya shambulio hilo, lakini chama cha mrengo wa kulia nchini India kinawalaumu wanamgambo wa kiislamu kwa kufanya hujuma hiyo. Chama kikuu cha upinzani nchini humo kimeitisha maandamao ya kitaifa nchini kote.