1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Azerbaijan: Urusi kuwaadhibu waliohusika na ajali ya ndege

30 Desemba 2024

Azerbaijan imesema leo Jumatatu kuwa serikali ya Urusi imeahidi kuwaadhibu wale waliohusika na kuangusha ndege ya Shirika la Ndege la Azerbaijan ambayo Azerbaijan inaamini ilidunguliwa na walinzi wa anga wa Urusi.

https://p.dw.com/p/4ogx4
Kasachstan | Aktau Flugzeugabsturz Azerbaijan Airlines
Video inaonyesha mabaki ya ndege ya Azerbaijan Airlines Embraer 190 karibu na Uwanja wa Ndege wa Aktau.Picha: The Administration of Mangystau Region/AP/dpa/picture alliance

Ndege hiyo ya shirika la ndege la Azerbaijan ilianguka Kazakhstan mnamo Disemba 25, na kuua watu 38 kati ya 67 waliokuwa ndani. Rais wa Azerbaijan Ilham Aliyev ameitaka Moscow ikubali kuwajibika kwa kuidungua ndege hiyo kimakosa ilipojaribu kutua katika uwanja wa ndege wa Grozny kusini mwa Urusi. Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Azerbaijan amesema katika taarifa yake leo kwamba mkuu wa Kamati ya Uchunguzi ya Urusi amewaambia kwamba Urusi inachukua hatua kali kuwabaini watu walio na hatia na kuwafikisha kwenye mikono ya sheria. Siku ya Jumamosi, Rais wa Urusi Vladmir Putin aliomba msamaha kwa Aliyev baada ya ajali hiyo ililiyotokea karibu na mji wa pwani wa Aktau nchini Kazakhstan.