1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mke na mume wafungwa zaidi ya miaka 30 kwa mauaji ya mtoto

18 Desemba 2024

Mahakama moja ya Uingereza imetoa hukumu ya kifungo cha maisha kwa baba na mama wa kambo wa mtoto wa miaka 10 raia wa Uingereza mwenye asili ya Kipakistani aliyekufa baada ya kuteswa kwa muda mrefu.

https://p.dw.com/p/4oGhN
UK | Gefängnis Wandsworth nach Flucht von Terrorverdächtigem
Kuta za mawe za Gereza la HM Wandsworth katika majira ya joto kusini mwa London Septemba 7, 2023.Picha: Justin Tallis/AFP/Getty Images

Urfan Sharif, mwenye umri wa miaka 43, amehukumiwa kifungo cha miaka 40, huku mkewe Beinash Batool, mwenye umri wa miaka 30, akihukumiwa kifungo cha miaka 33 kwa mauaji yaSara Sharif. Mahakama hiyo ilielezwa kuwa mwili wa Sarah ulipatikana ukiwa na majeraha makubwa akiwa amevujika baadhi ya viungo vya mwili pamoja na kuwa na majeraha ya kuchomwa na pasi. Jaji John Cavanagh amesema Sarah alikuwa muathirika wa mateso ya kupitiliza na kwamba Sharif na Batool hawakuonesha dalili zozote za kujutia matendo yao. Alikutwa akiwa amekufa kitandani mwake mwezi Agosti mwaka 2023 akiwa peke yake nyumbani. Uchunguzi wa maiti umeonyesha kuwa Sara alikuwa na majeraha 71 na kuvunjika mifupa mara 25.  Mjomba wake, Faisal Malik, aliye na umri wa miaka 29, pia alipatikana na hatia ya kusaidia au kuruhusu mauaji hayo kutokea na amehukumiwa kifungo cha miaka 16.