1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BAGHDAD: Naibu waziri wa afya wa Irak amekamatwa

8 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCU6

Vikosi vya usalama vya Marekani na vya Irak vimevamia wizara ya afya mjini Baghdad na vimemkamata naibu waziri,Hakim Zamili.Hayo ni kwa mujibu wa msemaji wa wizara ya afya.Maafisa wa majeshi ya Kimarekani bado hawakusema cho chote kuhusu ripoti hiyo.Zamili anajulikana kama ni mfuasi wa shehe alie na siasa kali-Moqtada al-Sadr.Kwa upande mwingine,zaidi ya watu 20 wameuawa katika mashambulio mbali mbali.Kwa mujibu wa polisi,watu 7 waliuawa mjini Baghdad baada ya bomu kuripuka karibu na basi moja.Na katika mji wa Aziziya,wanakoishi Washia wengi,si chini ya watu 15 walipoteza maisha yao katika mripuko wa bomu lililotegwa ndani ya gari.Vile vile wanajeshi 7 wa Kimarekani wamefariki katika ajali ya helikopta iliyotokea katika wilaya ya Anbar.Marekani imepoteza helikopta tano katika kipindi cha majuma matatu.