1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BAGHDAD: Wafungwa kuachiliwa huru mfungo wa Ramadhani

13 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBQA

Maafisa wa majeshi ya Marekani nchini Irak, wametangaza mpango wa kuanza kuwaachilia huru kati ya wafungwa 50 hadi 80 kila siku ya mwezi huu mtakatifu wa Ramadhan.Kwa Wasunni walio wachache nchini Irak,mwezi wa Ramadhan umeanza leo Alkhamisi na kwa Washsia walio wengi nchini humo,kesho Ijumaa ni mwanzo wa mfungo mtakatifu wa Ramadhan.Taarifa ya majeshi ya Marekani imesema,bodi maalum itachunguza nani atanufaika na mpango huo.Kiasi ya wafungwa 20,000 wamezuiliwa katika jela zinazosimamiwa na Marekani nchini Irak.