BAMAKO: Rais wa Guinea amemteua waziri mkuu mpya
27 Januari 2007Rais Lansana Conte wa Guinea anaekabiliwa na upinzani nchini,amekubali kumteua waziri mkuu mpya atakaekuwa na usemi mkubwa.Makubaliano hayo kati ya rais Conte na viongozi wa vyama vya wafanyakazi huenda yakasaidia kumaliza mgomo mkuu wa majuma mawili uliosababisha vifo vya si chini ya watu 60.Nchi hiyo ya Afrika Magharibi haina waziri mkuu tangu mwezi wa Aprili mwaka jana, baada ya rais Conte kumfukuza kazi kiongozi wa serikali.Wananchi wa Guinea kwa maelfu na elfu baada ya kuanza kuandamana tarehe 10 mwezi wa Januari kulalamika dhidi ya matatizo magumu ya kiuchumi,viongozi wa vyama vya wafanyakazi walitoa mwito wa kuchaguliwa waziri mkuu mpya. Waandamanaji wengi vile vile wametoa mwito wa kumtaka rais Conte ajiuzulu.Conte anatawala nchini Guinea tangu mwaka 1984.