Baraza la katiba Msumbiji yathibitsiha ushindi Daniel Chapo
23 Desemba 2024Matangazo
Baraza la Katiba ndilo lenye uamuzi wa mwisho kuhusu mchakato wa uchaguzi na uamuzi wake huenda ukachochea zaidi maandamano katika nchi hiyo ya kusini mwa Afrika yenye karibu watu milioni 35. Kiongozi wa upinzani ameapa kuendeleza "vurumai" ikwapo chama tawala kingethibitishwa kuwa mshindi katikati ya mzozo ambao tayari umegharimu maisha ya watu 130. Mwanasiasa wa Frelimo, Daniel Chapo sasa anatarajiwa kuchukua nafasi ya Rais Filipe Nyusi ambaye muhula wake wa pili unamalizika Januari 15.