1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Barnier atarajiwa kujiuzulu kama waziri mkuu wa Ufaransa

5 Desemba 2024

Waziri Mkuu wa Ufaransa Michel Barnier anatarajiwa kujiuzulu leo baada ya wabunge wa mrengo mkali wa kulia na wa kushoto kupiga kura kuiondoa madarakani serikali yake. miezi sita.

https://p.dw.com/p/4nm2S
Ufaransa | Paris 2024 | Waziri Mkuu | Michel Barnier
Waziri Mkuu wa Ufaransa Michel BarnierPicha: Sarah Meyssonnier/REUTERS

Kura hiyo ya wabunge imeitumbukiza Ufaransa katika mgogoro wake wa pili wa kisiasa katika kipindi cha katika kipindi cha miezi sita.

Barnier, mwanasiasa mkongwe ambaye pia aliongoza mazungumzo ya Uingereza kujiondoa kwenye Umoja wa Ulaya, Brexit, atakuwa waziri mkuu aliyehudumu kwa kipindi kifupi zaidi katika historia ya sasa ya Ufaransa.

kuongoza mazungumzo ya Uingereza kujitowa kwenye Umoja wa Ulaya, Brexit.

Soma pia: Wabunge waiangusha serikali Ufaransa

Hakuna serikali ya Ufaransa ambayo iliondolewa madarakani kwa kura ya bunge ya kutokuwa na imani nayo tangu serikali ya Georges Pompidou mnamo mwaka 1962.

Mirengo hiyo miwili ilimuadhibu Barnier kwa kutumia madaraka yake maalum ya kikatiba kutekeleza sehemu ya bajeti ambayo haiungwi mkono na umma bila ya kupata idhini ya bunge.

Rasimu ya bajeti hiyo ilikuwa inataka euro bilioni 60 ili kuziba pengo katika nakisi ya bajeti.

Kujiuzulu kwa Barnier kutamaliza wiki kadhaa za mvutano kuhusu bajeti, ambayo chama cha siasa kali za mrengo wa kulia cha National Rally cha Marine Le Pen, kimesema ilikuwa kali sana kwa wafanyakazi.