1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Basi la Borussia Dortmund lashambuliwa

11 Aprili 2017

Mechi ya ligi ya mabingwa barani Ulaya, Champions League, kati ya Borussia Dortmund na Monaco, ilikuwa ichezwe leo (11.04.2017) katika uwanja wa Signal Iduna Park mjini Dortmund.

https://p.dw.com/p/2b5AG
Borussia Dortmund Teambus nach Explosionen
Picha: picture-alliance/AP Images/M. Meissner

Basi la timu ya Borussia Dortmund limeharibiwa na abiria mmoja kujeruhiwa baada ya milipuko mitatu kutokea karibu na basi hilo lililokuwa njiani kuelekea uwanja wa Signal Iduna Park umbali wa kiasi kilometa kumi ambako mechi ya ligi ya mabingwa, Chamiopns League, ilitarajiwa kuchezwa. Tukio hilo limetokea mwendo wa saa moja usiku saa za Ujerumani.

Msemaji wa jeshi la polisi katika jimbo la North Rhine Westphalia, Gunnar Wortmann, aliliambia shirika la habari la Associated Press, "Basi lilianza safari kutoka hoteli ya timu ya Dortmund wakati milipuko mitatu ilipotokea. Milipuko mitatu ilitokea karibu na basi hilo lilipokuwa njiani kuelekea uwanjani na kwamba mchezaji mmoja amejeruhiwa na dirisha moja kuharibiwa."

Beki wa Dortmund ajeruhiwa

Fußball Bundesliga Borussia Dortmund - FC Ingolstadt 04 Marc Bartra
Beki wa Dortmund, Marc BartraPicha: picture-alliance

Gazeti la Ujerumani la Bild limeripoti kwamba beki wa Borussia Doetmund Marc Bartra amejeruhiwa na kupelekwa hospitali. Klabu ya Dortmund imetuma taarifa katika mtandao wa kijamii wa Twitter ikisema mchezaji huyo yuko salama na hakuna kitisho chochote ndani na nje ya uwanja wa Signal Iduna Park.

Mkurugenzi wa klabu ya Dortmund, Hans-Joachim Watzke, alithibitisha kujeruhiwa kwa Bartra, akisema ameumia mkononi na kuwa majeruhi si hatari kwa maisha yake. 

Msemaji wa polisi ya Dortmund, Nina Vogt, alisema wachunguzi bado hawafahamu chanzo cha milipuko iliyotokea wakati timu ya Borussia Dortmund ilipokuwa ikijiandaa kuondoka hotelini kuelekea uwanjani kuchuana na Monaco. Polisi imesema inalichukulia tukio hilo kuwa shambulizi. Hata hivyo hakuna dalili kuonyesha ni shambulizi la kigaidi.

Explosion am BVB Bus
Basi la Borussia Dortmund likionekana hapa baada ya mlipuko karibu na hoteli ya timu hiyo kabla mechiPicha: Reuters/K. Pfaffenbach

Dortmund iliamua kuiaharisha mechi hiyo ya duru ya kwanza ya robo fainali ya ligi ya mabingwa barani Ulaya na kuutangaza uamuzi huo kupitia ukurasa wake wa Twitter ikiongeza kuwa tiketi zote za mashabiki waliotaka kuutazama mtanange huo zinabaki kuwa halali na zitatumika kesho.

Mwandishi:Josephat Charo/dpa/ape/afpe/reuters