Bayajida - baba wa kabila la Hausa
Wanahistoria wanashaka kwamba Bayajida alikuwa kiumbe wa kweli, lakini hekaya za Bayajida bado ni imara. Zinamweleza kama mtu ambaye ukoo wake ndio ulioasisi taifa la Hausa. Mabadiliko muhimu katika jamii yanahusishwa na yeye, na hekaya hizo zinaadhimishwa kila mwaka mjini Daura, nchini Nigeria.
Ni wakati gani Bayajida aliishi?
Sehemu kubwa ya hekaya za Bayajida ilielezewa kupitia historia ya mazungumzo. Hakuna rekodi ya tarehe aliyozaliwa Bayajida ama kifo chake, na hakuna uhakika wa kuwapo kwake. Anaaminika kuwa alitokea Baghdad katika nchi ya sasa ya Iraq, na baada ya kukutana kwa muda na himaya ya Kenem mjini Bornu, aliweka makaazi yake Daura, ambao sasa ni Katsina.
Lakini nini hasa chanzo cha hekaya hii?
Baadhi ya vyanzo vinaeleza kwamba hekaya za Bayajida zinaonekana mahali fulani kati ya karne ya 16 na 19, wakati tayari kulikuwa na ushahidi wa kuishi kwake katika utamaduni wa Wahausa kati ya karne ya 9 na 10.
Nini maana ya jina lake?
Jina lake la asili huenda lilikuwa Abu Zaid. Jina hilo alilopewa na wahausa, Bayajida , kwa hakika ni neno: "Ba ya ji da" , likiwa na maana "aliyekuwa kwanza haelewi".
Nilisikia kuhusu mvuto kwa nyota hadithi inasemaje ?
Bayajida anasemekana kwamba alimuuwa nyoka ambaye aliishi kisimani kijijini Kusugu, sehemu ambayo ni Daura ya sasa. Nyoka huyo alikuwa akiwasumbua watu na kuwazuwia kuteka maji, nyoka huyo aliruhusu watu kuchota maji kutoka katika kisima hicho siku ya Ijumaa tu. Mbali na tahadhari zilizotolewa kwake, Bayajida alikwenda kuchota maji katika kisima hicho siku ya Alhamis. Wakati nyoka alipomshambulia, Bayajida alikwenda kuchota maji katika kisima hicho siku ya Alhamis. Nyota alipomshambulia , alimkata kichwa chake kwa upanga.
Hadithi yake ina mwisho mzuri?
kama zawadi ya kumuua nyoka, malkia wa Daura, Daurama aliahidi kumpa nusu ya ufalme wake . Lakini Bayajida kwa werevu alikataa na badala yake alimuomba malkia amuoe. Hii ilikuwa haijawahi kutokea, kwa kuwa malkia wote hubaki bila kuolewa maisha yake yote. Hata hivyo , Daurama alikubali kwa kuwa alijihisi ana deni kwake.
Nini alichokiacha:
Bayajida anajulikana kwa kubadilisha utamaduni katika ufalme wa daura: Kabla ya kuwasili, katika ufalme wa Daura ulikuwa unatawaliwa tu na wanawake. Utamaduni ulibadilika kutoka utawala wa wanawake hadi utawala wa wanaume baada ya kumoa malkia daurama na watoto wake wa kiume walirithi utawala wake.
Taifa la Hausa:
Bayajida alipata watoto watatu wa kiume: mke wake wa kwanza (mtoto wa mtawala wa ufalme wa Borno) alimuita Biram, mmoja wa malkia Daurama, aliyeitwa Bawo, na mmoja wa mahawara. Bawo alipata watoto sita wa kiume, ambao , pamoja na mjomba wao Biram, walikuja kuwa watawala majimbo halali saba ya Hausa ambayo yanafahamika kufuata : Daura, Kano, Katsina, Zaria, Gobir, rano na Hadeja.
Mwandishi: Sekione Kitojo
Mhariri: Yusuf Saumu
Pinado Abdu-Waba, Abdoulaye Mamman Amadou na Gwendolin Hilse wamechangia kuandika makala hii. Ni sehemu ya makala maalum za mfululizo wa "Asili ya Afrika", ushirikiano kati ya shirika la DW na taasisi ya Gerda Henkel.