1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bayern inaikaribisha Manchester City

26 Septemba 2011

Bayern Munich inaikaribisha hapo kesho Manchester city ya Uingereza katika mashindano hayo kwenye kundi A

https://p.dw.com/p/12gma
Ni sherehe baada ya ushindiPicha: AP

Bayern inatambua kuwa ushindi dhidi ya Manchester City inayoonekana kuwa mpinzani mkuu kwenye kundi hilo, utaiweka Bayern kwenye usukani wa kundi hilo.

Jerome Boateng wechselt zum FC Bayern München
Jerome Boateng alipokuwa akiichezea Manchester City sasa yuko na Bayern MunichPicha: picture alliance/dpa

Ni mechi ya pili kwa Bayern kwenye kundi hilo na inaelekea kushiriki mechi ya hapo kesho ikiwa katika shauku kubwa baada ya kufanikiwa kushinda mechi zake tisa za nyuma katika mashindano yake yote pasi kufungwa hata bao moja.

Pia walishinda mechi yao ya kufungua mashindano hayo ya makundi dhidi ya Villareal wiki iliyopita na kuongoza katika pointi.

Licha ya kuwa kuna historia kati ya timu hiyo kuu ya Ujerumani na mji wa Manchester Uingereza, Bayern imehusika zaidi na timu ya Manchester United na siyo City.

Sport Fussball Champions League FC Villarreal gegen FC Bayern München
Bayern Munich dhidi ya Villarreal, timu za Kundi A kwenye champions leaguePicha: dapd

Hatahivyo kama walivyosema waswahili kuwa yaliyopita si ndwele tugange yajayo, ndiyo msimamo pia wa Bayern maana ina hamu ya kutizama mechi zinazokuja kuliko zilizopita, na kwa kuwa fainali za mashindano haya zitafanyika mjini Bayern kwenyewe, timu hiyo ina hamu ya kujaribu kujinyakulia taji hilo kwa mara ya tano.

Katika mechi ya kesho, Bayern inamshirikisha winga Arjen Robben aliyekuwa nje kutokana na maumivu tangu mwezi Agosti. Mario Gomez pia anatarajiwa kuwepo katika kikosi cha kwanza baada ya kucheza dhidi ya Leverkusen mwishoni mwa juma na hii ni baada ya yeye pia kukosekana kutokanana maumivu pia.

Afisa mkuu mtandaji wa timu hiyo, Karl Heinz Rummenige, ameeleza kuwa kikosi kizima kimejitayarisha vilivyo na kuna matumaini makubwa.

Fussball Bundesliga Saison 10/11 20. Spieltag Werder Bremen FC Bayern München
Arjen Robbenwa Bayern MunichPicha: AP

Ama kwa upande wa timu hyo ya Uingereza hata nayo inaelekea kwenye mechi ya kesho ikiwa na imani baada ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Everton mwishoni mwa juma na ikiwa na pointi sawa na jirani yake mpinzani Manchester United katika ligi ya Uingereza, Premier League.

City tayari mpaka sasa imefunga mabao 19 katika mechi 6 katika msimu mpya wa Premier league ambao hawajafungwa, huku mfungaji Sergio Aguero raia wa Argentina akiwa ndiyo wa kutizamwa kutokana na kufanikiwa kwake kuifungua City mbao 8 katiy a hao 19.

Kwengineko Timu ya Uhispania, Real Madrid, inajitayrisha kuikaribisha Ajax Amsterdam hapo kesho pia katika kundi D, na rais wa Real Florentino Perez anaamini kumuajiri kocha Jose Mourinho na kutumia mamilioni ya fedha kwa wachezaji wake tayari kumeweka msingi wa ushindi wa taji hilo la Ulaya kwa mara ya kumi kwa timu yake.

Özil Coruna
Mesut Özil wa Real MadridPicha: picture-alliance/EXPA/Alterph

Real ilianza kampeni yake ya ushindi wa taji hili kwa kuifunga Dinamo Zagreb 1-0 katika mechi yake ya kwanza kwenye kundi hilo na imejitayarisha kwa mechi ya hapo kesho kwa mazoezi uwanjani Bernabeu mwishoni mwa juma katika ligi ya Uhispania na kuifunga jirani Rayo Vallecano mabao 6-2.

Mbrazil anayecheza kiungo cha beki kushoto, Marcello, atakosekana hapo kesho baada ya kufukuzwa katika mechi dhidi ya Zagreb na pia Wareno Pepe na Fabio Coentrao walio nje kutokana na maumivu.

Mwandishi: Maryam Abdalla/Rtre
Mhariri: Abdul-Rahman