1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bayern kupambana na Schalke 04

16 Septemba 2011

Kipa wa Bayern Munich Manuel Neuer huenda asipokee mapokezi mema hapo kesho wakati timu yake itakapokabiliana na timu yake ya zamani Schalke 04 kwa mara ya kwanza tangu aihamie Bayern Munich.

https://p.dw.com/p/12adj
Kibarua kigumu kinamsubiri Manuel NeuerPicha: dapd

Manuel Neuer anaonekana kufanikiwa kuwashawishi mashabiki wa Bayern waliokuwa wakipinga usajili wake mwishoni mwa msimu uliopita.

Eintracht Braunschweig - Bayern München DFB-Pokal Saison 2011/12
Picha: dapd

Sasa anakabiliwa na hisia kama hizo kutoka kwa mashabiki wa Schalke wanao ona kuwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25, aliwasaliti kwa kujiunga na timu hasimu.

Mechi ya hapo kesho itakuwa ni ya pili kwake kushiriki katika uwanja wa Veltins Arena tangu aihamie Bayern.

Mchezaji mwenzake wa zamani na rafiki yake, Benedikt Howedes amesema anatarajia Neuer akabiliwe na upinzani kutoka kwa mashabiki lakini anatarajia kuwa mashabiki wengi watamkaribisha vizuri kipa huyo.

Timu ya Bayern ipo imara na thabiti baada ya kurudi kutoka ushindi dhidi ya Villareal walikoifunga timu hiyo mabao 2-0 katika mashindano ya kuwania ubingwa Ulaya.

Huku nayo Schalke inatarajiwa kufufuka kutoka mpambano wa mashindano ya ligi ya Europa dhidi ya Steaua Bucharest siku ya alhamisi wiki hii walikotoka sare ya 0-0.

1. FSV Mainz 05 gegen FC Schalke 04
kikosi cha Schalke 04 uwanjaniPicha: picture alliance/dpa

Mfungaji nambari moja kwenye ligi ya Ujerumani Mario Gomez aliyefunga mabao 4 dhidi ya Freiburg Jumamosi iliyopita na mlinzi Daniel van Buyten ni wachezaji ambao huenda wasishiriki katika mechi ya kesho baada ya kutolewa kwenye mechi hiyo nchini Uhispania.

Bayern ipo katika kiwango sawa juu ya orodha ya ligi hiyo na Werder Bremen ambao nao hii leo wanaonana na Nuremberg na kuwania kuendelea na mwanzo uliyowashangaza wengi kufuatia kujikokota kwake msimu uliyopita.

Kufuatia sare ya bao 1-1 na timu ya Uingereza Arsenal katika mashindano ya Champions league, timu bingwa Borussia Dortmund imempoteza mchezaji wake wa kiungo cha kati Sven Bender kufuatia maumivu aliyopata kabla ya mechi ya hapo kesho dhidi ya Hanover 96.

Mario Goetze na Kapteni Sebastian Kehl wanaocheza kiungo cha kati, wote wametolewa kutoshiriki mechi hiyo huku Lucas Barrios bado yupo nje kutokana na maumivu wakati timu hiyo bingwa mtetezi inajaribu kufufuka kutoka kushindwa nyumbani na Hertha Berlin.

Bayer Leverkusen nayo iliyopo nyuma ya Bayern na Werder Bremen kwa pointi mbili, inashindana na Cologne katika mechi ya nyumbani wakati nayo Borussia Monchengladbach iliyo katika kiwango sawa na Leverkusen, inaitembela timu iliyopo mwisho Hamburg.

BuLi Hamburger SV vs Hertha BSC 2011
Marcell Jansen na David Jarolim wa timu ya Hamburg SVPicha: dapd

Hii leo pia Hoffenheim inaikaribisha Wolfsburg, Hertha Berlin inakuwa mwenyeji wa Augsburg na Mainz inaitembelea Kaiserslautern.

Na hii leo kunafanyika mashindano ya kwanza ya riadha mwaka huu mjini Kampala Uganda yanayowashirikisha wanafunzi wa taasisi mbalimbali zikiwemo shule na vyuo vikuu, vilabu na kampuni,pamoja na watu binafsi.

Mashindano hayo yanafanyika nje ya chuo kikuu cha Makerere mjini Kampala na yanaanza mwendo wa saa mbili kamili kwa saa za afrika mashariki.

Kufikia jana jioni shirikisho la riadha Kampala ambalo linasimamia mashindano hayo lilisema kuwa ni watu 100 waliokuwa wamejisajili kushiriki katika mbio hizo leo hata hivyo idadi hiyo inatarajiwa kuongezeka hii leo.

Akizungumza na DW kupitia njia ya simu mwenyekiti wa shirikisho hilo la riadha Kampala, Geoffrey kagwa alisema kuwa mashindano haya yameanadaliwa kuwatayarisha wanafunzikwa mahsindnao mengine yanayowadia.

Washindi wa tatu wa kwanza watapokea zawadi ya kitabu kinachoeleza zaidi kuhusu riadha.

Mwandishi:Maryam Abdalla/Rtre/Dpae/Afpe
Mhariri:Josephat Charo