1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bayern kuumana na Dortmund katika DFB Pokal

Admin.WagnerD27 Aprili 2015

Baada ya kuhifadhi Ubingwa wa Bundesliga, Bayern Munich bado inakabiliwa na kibarua kingine dhidi ya Borussia Dortmund katika nusu fainali ya kombe la shirikisho DFB Pokal mjini Munich

https://p.dw.com/p/1FFnc
Fußball 1. Bundesliga 27. Spieltag Borussia Dortmund - Bayern München
Picha: Patrik Stollarz/AFP/Getty Images

Bayern Munich inawania kutawazwa mabingwa wa mataji matatu msimu , katika kombe hilo na pia Champions League ambapo inapambana na Barcelona katika nusu fainali.

Mpambano wa kesho wa DFB Pokal unatarajiwa kuwa wa hamasa kubwa , ambapo Bayern na Dortmund kwa mara nyingine tena zinapimana ubavu katika kile ambacho kimekuwa mpambano wa wababe wawili katika misimu michache iliyopita.

Bayern iliishinda Dortmund katika muda wa ziada katika fainali ya msimu uliopita, ikilipiza kisasi kwa kufungwa mabao 5-2 katika fainali ya mwaka 2012 katika uwanja wa Olimpiki mjini Munich. Jumatano ni zamu ya VFL Wolfsburg ikipambana na timu ya daraja la tatu ya Armenia Bielefeld katika nusu fainali nyingine.

Mwandishi: Sekione Kitojo / afpe / ape / rtre
Mhariri: Yusuf , Saumu