Schweinsteiger ajiunga na Manchester United
12 Julai 2015Hata hivyo mkurugenzi mkuu mtendaji wa Bayern Munich Karl-Heinz Rummenigge amekiri kuwa tayari Manchester United wamewasiliana nao. Schweinsteiger amecheza mechi 536 tangu ajiunge na klabu hiyo ya Bayern mwaka wa 2002.
Rummenigge amesema inahuzunisha sana kwani Bastian alikuwa ni kigogo wa timu ya Bayern na wangemtaka sana aendelee kuwachezea mabingwa hao.
Schweinsteiger amekuwa Bayern Munich kwa miaka 17. "ametufanyia mambo mengi mazuri tu kwa hivyo alipoomba ruhusa ya kuondoka hatukuwa na budi'' Alisema Rummenige
''Kwetu ni heshima kwani ametuhudumia kwa miaka 17 kwa hivyo tukamuacha aendee akastaafie Uingereza'' alisema Rummenigge
Kocha wa Man Utd Louis van Gaal amekuwa shabiki wa Schweinsteiger tangu mwaka wa 2009 – 2011 wakati alipoingoza klabu hiyo katika fainali ya Champions League ya mwaka wa 2010.
Mwandishi: Bruce Amani/AFP
Mhariri: Mohamed Dahman