Bayern Munich ina miadi na Olympique Lyon
9 Desemba 2008Baada ya jana Werder Bremen kuaga rasmi kombe la ulaya la UEFA kwa changamoto nyumbani na Inter Milan ya Itali, leo macho yanakodolewa kwa mabingwa wa Ujerumani Bayern Munich ambao pamoja na mabingwa watetezi Manchester united,Real Madrid ya Spian,Juventus ya Itali na Arsenal London zina uhakika wa kucheza duru ijayo.Real Madrid yasemekana imeshavionjari kumtimua kocha wao mjerumani Bernd Schuster na jina la kocha mpya linalovuma ni lile la Juande Ramos.
Mabingwa wa Ulaya Manchester united wana miadi leo na Aalborg na tiketi yao ya duru ijayo, tayari iko kibindoni.Celtic ya Scotland inacheza nyumbani na mahaysimu wao ni waspain Villarreal.Mabingwa wa Ujerumani bayern munich wakitamba katika kundi F wanawasili leo Ufaransa kwa miadi yao na Olympique Lyon.Munich sio tu imeshatia mguu duru ijayo ya kombe hili la ulaya, bali imerudi kutamba nyumbani katika Bundesliga.Mpambyano wake wa leo unafuatia ushindi wake wa dakika ya mwisho wa mabao 2-1 dhidi ya Hoffenheim,mpambano ulioangaliwa na mashabiki kutoka nchi 168 ijumaa iliopita. Iwapo munich itathubutu pia kutamba leo nyumbani mwa Lyon ,tusubiri kuona.Salamu lakini,imeshatoa kwa Lyon na wenzake.Olympique Lyon iko nafasi ya pili katika kundi hili nyuma ya Bayern munich ikifuatwa na Fiorentina na Steua Bucharest.
Arsenal ya Uingereza inacheza leo na Porto ya Ureno huko Porto wakati Dynamo Kiev inatembelewa Ukrain na waturuki- Fenerbahce.Kileleni mwa kundi hili wako Arsenal huku Porto wakinyatia nafasi ya pili .
Changam,oto za kundi H ni kati ya Juventus na Borisov huku mabingwa mara kadhaa wa Ulaya Real Madrid wakipimana nguvu na Zenit St.Petersburg ya Russia.Juventus ndio inayoongoza kundi hili ikifuatwa na Real Madrid ambayo hatima ya kocha wake mjerumani Bernd Schuster huenda imeshakatwa:
Mkurugenzi wa rteal madrid Pedja Mijatovic alitisha mkutano na waandishi habari alaasiri ya jana huku uvumi ulipozagaa kwamba kocha wa zamani wa Tottenham Hotspurs ya uingereza na Sevilla ya Spain Juande Ramos ndie yuko usoni kabisa mwa majina ya kujaza nafasi ya Bernd Schuster,stadi wa zamani wa timu ya taifa ya ujerumani na Real.
Real ililazwa mwishoni mwa wiki kwa mabao 4-3 na sasa imeangukia nafasi ya 5 ya ngazi ya Ligi ya Spain.Kwahivyo, maji yamezidi unga na Real,klabu ilioweka rekodi katika kutwaa ubingwa wa kombe hili la Ulaya,haiwezi kuvumilia tena.Changamoto ya jioni hii na St.Petersburg,itaangaliwa kwa jicho maalumu.Kwani, jumamosi ijayo,Real madrid ina miadi na mahasimu wao wa jadi katika La Liga,Ligi ya Spian FC Barcelona.Real inaelewa ikishinda changamoto hiyo itafungua ukurasa mpya katika juhudi zake za kutawazwa mabingwa wa Spian msimu huu.FC Barcelona lakini, inatamba wakati huu,na ikiwa haijafungwa mapambano 20 katika mashindano mbali mbali, Real, ama chini ya kocha wa zamani au mpya, haitakua na kibarua rahisi.