Bayern Munich kukabidhiwa Taji la ubingwa leo
7 Mei 2010Bayern Munich, inakabidhiwa leo taji la Bundesliga-Ligi ya Ujerumani, mara tu ikimaliza mpmbano wa mwisho wa msimu na Hertha Berlin, huko Olympic Stadium.Kesho, itafahamika ama Chelsea au Manchester United, itatoroka na taji la Premier League.
Katika La Liga- ligi ya Spain, FC Barcelona inaongoza kwa pointi 4 mbele ya Real Madrid,lakini Real, bado haikukata tamaa ya taji la ubingwa.
Barani Afrika,kinyan'ganyiro cha Kombe lake la klabu bingwa na la Shirikisho, kinarudi uwanjani kwa mabingwa TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo, wakiikaribisha nyumbani, Lumbubashi, Djoliba ya Mali.
Katika Kombe la shirikisho, mabingwa wa Tanzania-Simba, wamejiwinda kutetea ushindi wao wa nyumbani wa mabao 2:1 dhidi ya Harras Al-Hodoud, mjini Alexandria,Misri.
Taji la Bundesliga jioni hii likielekea Munich, mashabiki wa Bayern Munich, wameshaanza shangwe na shamra shamra na jioni hii basi,"Asie na mwana ,aeleke jiwe na asie na mguu atie gongo" -mkutano Olympic Stadium,Berlin na mjini Munich kwenyewe.Kwani, sherehe za "Oktobafest" zimekuja mapema mwaka huu- mwezi Mei.
Kwa kweli, m pambano wa jioni hii na wenyeji Hertha Berlin, ni ada tu.Rasmi,Munich ililitwaa taji tayari Jumamosi iliopita ilipoizaba Bochum mabao 3:1.Schalke, iliokua ikinyan'ganyia taji na Munich iliteleza ilipochapwa nyumbani mabao 3 bila jibu na Werder Bremen. Waklati ule ingawa timu hizo 2 zilisimama pointi sawa, Munich ikiongoza kwa mabao 17.
Ikilipokea Kombe jioni hii, sherehe kwa Bayern Munich, hazitakuwa zimemalizika.Kwani,Itarudi Jumamosi ijayo kwa finali nyengine katika uwanja huo huo ya Kombe la Taifa.Halafu itasubiri Mei 22 mjini Madrid,kituo cha finali ya champions League na Inter Milan ya Itali.Bayern Munich, inalenga kutwaa vikombe vyote 3-viwili nyumbani na kimoja ulaya.
Werder Bremen, iliopo nafasi ya 3 ya ngazi ya Ligi, ina miadi leo na majirani zao Hamburg,ikijua ikishinda au kutoka sare leo, ittakata tiketi ya champions league-msimu ujao.
Kinyan'ganyiro pia kiko mkiani mwa ligi huku timu 3 zitajua leo hatima yao:Bochum,Hannover na Nüremberg. Nuremberg inacheza nyumbani na FC Cologne na lazima ishinde isalie daraja ya kwanza.Hali ni sawa na hiyo kwa Bochum ilipo nyumbani ikiumana na Hannover.
Katika Premier League,Chelsea, ina azma kesho kuigiza Bayern Munich na kuondoka uwanjani na taji:Ikiwa Chelsea,itaipiga kumbo Wigan Athletics, basi taji ni lao.Ikishindwa , Manchester United, waweza wao wakalibeba taji mradi nao watambe mbele ya Stoke City.
Huko Spain, FC Barcelona, imefungua mwanya wa pointi 4 kileleni kati yake na Real Madrid,ingawa Real, ina mpambano 1 zaidi kucheza.Barcelona ikiendelea kutamba na Lionel Messi, alietia bao lake la 31 kati ya wiki hii,ina inacheza leo na Sevilla wakati Real Madrid, ikitamba na Cristian Ronaldo , mahasimu wao jioni hii nyumbani ni Sevilla.
Mabingwa wa klabu bingwa TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo, wamejiwinda kuionesha Djoliba ya Mali,kile "kilichomtoa kanga manyoya". Mabingwa mara 6 wa Afrika Al Ahly ya Misri, wanaikaribisha nyumbani Cairo, Al-Ittihad ya Libya. tena kwa haluwa. Al Ahly ilipata pigo la kutoka Kano Pillars ya Nigeria, ilipotoka sare mara mbili mjini Kano na nyumbani Cairo.
Gabarone Utd. ya Botswana, inacheza na Dynamo ya Zimbabwe, wakati Zanaco ya Zambia , inachuana na Entete Setif ya Algeria kufuta bao 1 walilotiwa ugenini.
Ama katika Kombe la Shirikisho la dimba la Afrika-Confederation cup, Simba ya Tanzania, imejiwinda kunguruma huko Alexandria,Misri , na kutetea mabao yake 2:1 iliotia Dar-es-salaam.Klabu 2 za Nigeria-Enyimba na Warr Wolves, zinakumbana na kibarua kigumu katika duru ya 3 ya Kombe hili.
Enyimba mabingwa 2003 na 2004 wa Kombe la klabu bingwa,walipigwa vita kweli duru ya kwanza na kutolewa nje ya uwanja kwa mabao 3 na Vita Club ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo.Warri inaongoza kwa mabao 2:1 inapoingia uwanjani mjini Harare kupambana na C APS United.
Mwandishi: Ramadhan Ali /AFPE/DPAE/RTRE
Mhariri:Aboubakary Liongo