1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bayern Munich watwaa kombe la shirikisho

21 Aprili 2008

Bayern munich iko njiani kutimiza shabaha yake ya kutwaa vikombe 3 msimu huu-kombe la DFB,la Bundesliga na la UEFA.

https://p.dw.com/p/DljH
Wachezaji wa Munich washangiria Kombe.Picha: AP

Bayern Munich imeshatia kapuni moja kati ya vikombe 3 inavyolenga kubeba msimu huu-kombe la shirikisho la dimba la Ujerumani- Young Africans yatawazwa na mapema mabingwa Tanzania lakini bila hoi hoi kutoka kwa mashabiki-kisa nini ? Na

Mwenge wa olimpik ulipita leo Kuala Lumpur, mji mkuu wa malaysia chini ya ulinzi mkali.

Bayern Munich walitawazwa jumamosi mabingwa wa kombe la DFB-shirikisho la dimba la ujerumani baada ya kuizaba Borussia Dortmund mabao 2:1 .Ushindi huo lakini haukua wa mteremko kinyume na ule walioupata wiki moja kabla katika changamoto za Bundesliga walipoikomea Dortmund mabao 5:0.

Jumamosi Munich walitokwa na jasho kabla kutoroka na kombe.Kwani, baada ya kutia bao la kwanza na kudhania wameshashinda, Dortmund ilitia fora na dakika 1 kabla ya firimbi ya mwisho kulia, walisawazisha mnamo dakika ya 89 ya mchezo.Munich ikachachama katika kipindi cha kurefusha mchezo na katika dakika ya 13 ya mchezo Luca Toni, aliufumania tena mlango wa Dortmund kwa bao la ushindi.

Kwa ushindi huo,Munich imetimiza shabaha yake ya kwanza msimu huu ya kutwaa vikombe 3 kwa msimu mmoja:kombe hilo la shirikisho, kombe la Ligi na kombe la Ulaya la UEFA.

Kocha wa Munich Ottmar Hitzfeld ambae mwishoni mwa msimu huu anaiacha mkono B.Munich na kipa Oliver Kahn anastaafu-wote watafurahia vikombe hivyo vitatu. Kocha wa Munich Ottmar Hitzfeld mwishoe alisema:

"Ni zawadi nzuri kwa kuagana.nimefurahi kuona ulikua mchezo wa kusisimua.Dortmund ilicheza kwa nguvu sana na hata nao walistahiki kushinda."

Kwa Borussia Dortmund na kocha wao Thomas Doll,ingawa hawakuondoka na kombe, wameweza kufuta ile aibu waliopakwa wiki moja kabla na B.Munich walipozabwa mabao 5-0.Laiti bahati ingelia upande wao, wangeweza pia kuondoka na kombe.

Taarifa kutoka Gelsenkirchen, zasema Schalke huenda imejipatia kocha mpya nae ni Mholanzi Fred Rutten .Kwa muujibu wa taarifa anafunga mkataba na Schalke hadi 2010 na atakombolewa kutoka klabu yake ya sasa ya Enschede kwa kitita cha Euro nusu-milioni.Wiki iliopita, Schalke iliachana mkono na kocha wake Mirko Slomka.Kwa sasa hadi mwisho wa msimu huu ni Büskens na youri Mulder.

Katika serie A, Ligi ya itali, Inter Milan inaongoza kwa pointi 78 ikifuatwa nyuma na As Roma yenye pointi 72 huku Juventus Turin ikinyatia nafasi ya 3.Mwishoni mwa wiki As Roma ilimudu sare tu bao 1:1 na Livorno Calcio wakati viongozi wa Ligi Inter Milan ilitamba kwa bao 1:0 tu mbele ya FC Turin.

Katika la Liga au Ligi ya Spian-viongozi wa Ligi-Real mardrid wameendelea kupanua mwanya wao kileleni.Wakiongoza kwa pointi 72 kwa 62 za villareal yenye pointi 62.Barcelona inanyatia nafasi ya 3 kwani ilitoka suluhu tu 0:0 na Espanyol Barcelona.Real Madrid iliikomea Racing Santander mabao 2:0.

Am,a katika Ligi ya Ufaransa Olympique Lyon inaendelea kutamba kileleni ikiongoza Ligi hiyo kwa pointi 71 huku wapinzani wao Gorondins Bordeax ikifuata nafasi ya pili kwa pointi 67 na Nancy iko nafasi ya tatu kwa jumla ya pointi 55.

Young Africans ya Tanzania,imeshatawazwa mabingwa na mapema mwishoni mwa wiki.Lakini jinsi ilivyochezana kuondoka sare,kutawazwa huko mabingwa kabla msimu kumalizika hakukupokewa kwa shangwe na shamra shamra.

Wakati nchini Tanzania .Yanga wametamba,katika Ligi ya Kenya World Hope waongoza kileleni .

Mwenge wa olimpik ulipita leo mjini Kuala Lumpur,Malaysia leo hii katika hali ya ulinzi mkali.Polisi na vyombo vya usalama vilijitahidi mno kuzuwia fujo lililouandama mwenge huo mjini London,Paris na San Francisco.Polisi mjini Kuala Lumpur, iliwaonya waandamanaji wangetiwa nguvuni iwapo wangejaribu kuzusha fujo.Kiasi cha askari 1,000 waliweka usalama kandoni mwaka masafa ya km 16.5 ulipopitia mwenge huo.

►◄