1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BAYERN MUNICH YAKANDIKWA 3:1 NA BIELEFELD

14 Februari 2005
https://p.dw.com/p/CHZS

BAYERN MUNICH YACHEZESHWA KINDUMBWE-NDUMBWE NA BIELEFELD KATIKA BUNDESLIGA

MATOKEO YA KOMBE LA KLABU BINGWA BARANI AFRIKA

NA SAMUEL ETO’O ATARAJIWA KUTAWAZWA TENA KESHO ‘MCHEZAJI BORA KABISA WA DIMBA BARANI AFRIKA’.

Katika Bundesliga,kulizuka maajabu jana pale timu iliopanda daraja ya kwanza msimu huu-Armenia Bielefeld ikicheza na muafrika Kusini Delron Buckley iliichezesha jana Bayern Munich kindumbwe ndumbwe na kuikomea mabao 3:1.Kwanza alikua mtaliana Massimilian Porcello alieufumania mlango wa Oliver Kahn kwa bao la kwanza la Armenia Bielefeld mnamo dakika ya 23 ya mchezo.

Delron Buckley akaongeza bao la pili la Bielefeld pale mkwaju wake maridadi kabisa ulimpita Oliver Kahn ukielekea kmimiyani.Munich ikijaribu kufufuka, mbrazil Lucio aliipatia Munich bao kufuatia mkwaju maridadi wa freekick.Lakini haukupita muda, Delron Buckley akaufumania tena mlango wa Munich kwa bao la tatu.Kwa ushindi wa mabao 3:1,Bielefeld imifanya kile ambacho hakuna aliethbutu kutazamia ingelifanya-kuinyanganya pointi 3 Bayern Munich.

Hatahivyo, licha ya pigo hilo,Munich inaongoza orodha ya Ligi ingawa kwa magoli.Ina jumla ya pointi 41 sawa na Schalke ambayo ilitamba nyumbani ikicheza na Gerald Asamoah na kuizaba Wolfsburg mabao 3-0.

Mabingwa watetezi-Werder Bremen,wsalionyakua vikombe 2 msimu uliopita sasa wameangukia nafasi ya tatu ya ngazi ya Ligi baada ya kuipiku Stuttgart.Bremen waliondoka na ushindi wa mabao 2:0 dhidi ya Borussia Mönchengladbach.

Bayer Leverkusen imeparamia hadi nafasi ya 6 baada ya kuichapa Mainz mabao 2-0.

Kashfa ya marifu katika dimba la Ujerumani ilipata msukumo mpya mwishoni mwa wiki,pale rifu wa kwanza kuungama akipangilia matokeo katika mechi alizochezesha ili kuvuna vitita vyavfedha katika mchezo wa kamari –Robert Hoyzer kutiwa binafsi nguvuni na polisi.Hoyzer rifu mwenye umri wa miaka 25 alikamatwa jumamosi na polisi ambayo ikihofia angeweza kutoroka nchini.

Baada ya shirikisho la dimba la Ulaya-UEFA kuamua kutunga sheria maalum kuzagaa na kuathiri imani katika matokeo ya dimba, FIFA-shirikisho la kabumbu ulimwenguni nalo linazingatia sasa kuweka mada hii katika ajenda ya mkutano wa Halmashauri yake tendaji ili kuzuwia mtindo huu kuenea zaidi.

Rais wa FIFA Sepp Blatter amenukuliwa kusema, "Mkasa ulitokea Ujerumani ni bunduki iliofyatuliwa kutoa onyo ‘.