1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bayern wawazidi kete Dortmund Super Cup

1 Oktoba 2020

Joshua Kimmich alifunga goli la ushindi na Bayern Munich wakawazidi kete Borussia Dortmund 3-2 na kuebuka mabingwa wa Super Cup. Haya ni licha ya hofu kuwa wachezaji wa Bayern wamechoka kutokana na msongamano wa mechi.

https://p.dw.com/p/3jHGT
DFL-Supercup | Bayern Munich v Borussia Dortmund | Tor Bayern (3:2)
Picha: Christof Stache/AFP/Getty Images

Dortmund walikuwa wamefungwa 2-0 baada ya Corentin Tolisso na Thomas Müller kuwaweka mabingwa hao wa Ulaya uongozini.

Erling Haaland aliwapa BVB goli la kwanza kisha akaongeza la pili ilipotimu dakika ya 55. Ushindi huu wa Bayern umekuja baada ya kichapo cha magoli 4 walichopokea katika Bundesliga mwishoni mwa wiki iliyopita mikononi mwa TSG Hoffenheim.

DFL-Supercup | Bayern Munich v Borussia Dortmund | Tor Dortmund (2:2)
Erlind Haaland akipongezwa na wachezaji wenzake baada ya kufunga goli la kwanza la DortmundPicha: Andreas Gebert/Reuters

Mechi hiyo ambapo mshambuliaji wa Hoffenheim Andrej Kramaric alipachika wavuni magoli mawili imezua tetesi kwamba Bayern sasa wanamuwinda mshambuliaji huyo raia wa Croatia. Ripoti zinaarifu kwamba Bayern wanamtaka Kramaric awe msaidizi wa mshambuliaji wao Robert Lewandowski ambaye alighadhabishwa sana na kushindwa huko mnamo Jumapili.

Gazeti la kila siku la Ujerumani Bild limeripoti kuwa mkurugenzi wa michezo wa klabu hiyo Hassan Salihamidzic aliwasiliana na wakala wa Kramaric baada ya kipigo hicho cha Jumapili.