Bayern yafungwa lakini yasonga mbele
24 Novemba 2010Bayern Munich ilikuwa inaongoza katika nusu ya kwanza ya mchezo baada ya mshambuliaji wake Mario Gomez kuifungia timu yake hiyo mabao mawili.
Lakini baadae katika nusu ya pili ya mchezo, AS Roma ilifanikiwa kujipatia ushindi huo wa mabao 3-2. Bayern Munich ambayo tayari imepitia katika awamu ya mtoano, kwa sasa inaongoza kundi E ikiwa na pointi tatu.
Katika mechi nyingine Basel iliifunga CFR Cluj bao 1-0, huku Olympique Marseille ikiichapa Sptartak Moscow mabao 3-0.
Chelsea ambayo tayari imekwishafuzu kwa raundi ijayo iliendeleza ubabe wake kwa kuifunga Zilina mabao 2-1.Nayo AC Milan ilitamba ugenini kwa kuichapa Auxerre mabao 2-0.
Real Madrid haikuwa na huruma kwa Ajax Amsterdam pale ilipoishindilia mabao 4-0, il hali Arsenal ikilambishwa mchanga na Braga kwa kufungwa mabao 2-0.Shakhtar Donetsk ilitamba ugenini kwa ushindi wa mabao 3-0 mbele ya Partizan Belgrade.
Mwandishi:Aboubakary Liongo/Reuters