1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bayern yasitisha mazungumzo ya mkataba na Alaba

2 Novemba 2020

Mshindi mara mbili wa Champions League David Alaba anaelekea kuondoka klabu hiyo baada ya miamba hao kusema kuwa mazungumzo kuhusu mkataba mpya yamevunjika. Mkataba wake unakamilika mwishoni mwa msimu huu.

https://p.dw.com/p/3klxx
UEFA Champions League | Bayern München vs. Ajax Amsterdam
Picha: Reuters/A. Gebert

Rais wa klabu hiyo Herbert Hainer amenukuliwa na chombo kimoja cha habari Ujerumani akisema kuwa Bayern iliweka mwishoni mwa Oktoba kuwa muda wa mwisho kwa Muastria huyo na wakala wake kujibu ofa nzuri kabisa ya mkataba mpya, na baada ya muda huo kuisha bila makubaliano, ofa hiyo ikaondolewa.

"Baada ya hapo tuliamua kuondoa kabisa ofa hiyo mezani. Hiyo ina maana hakuna ofa nyingine ndefu." Amesema Hainer.

Alaba anayeweza kucheza kama mlinzi au kiungo ameichezea Bayern mechi 271 tangu alipojiunga nao kama mchezaji chipukizi mwaka wa 2008. Ameshinda mataji tisa ya Bundesliga. Mkataba wake unakamilika mwishoni mwa msimu huu.

Reuters, AFP, AP, DPA