Bayern yatetea taji.
16 Desemba 2007Matangazo
Michezo.
Bayern Munich imefanikiwa kutetea uongozi wake katika ligi daraja la kwanza nchini Ujerumani Bundesliga na kuingia katika kipindi cha mapumziko ya majira ya baridi kwa kutoka sare ya bila kufungana na Hertha BSC Berlin. Lakini Werder Bremen iliweza kuwa sawa kwa points 36 na Bayern baada ya kuibamiza Bayer Leverkusen kwa mabao 5-2. Mabingwa Stuttgart waligaragazwa kwa mabao 2-0 na Arminia Bielefeld. Schalke 04 imesogea hadi nafasi ya tano kwa ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Nuremberg. Katika michezo mingine siku ya Jumamosi Karlsruhe ilitoka sare ya bao 1-1 na Hamburg na Wolfsburg ikaichaanga bakora Borussia Dortmund 4-0.