1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bayern yaweka historia Ujerumani

2 Juni 2013

Bayern Munich imekuwa klabu ya kwanza ya Ujerumani kushinda mataji matatu katika msimu mmoja, baada ya kuifunga VfB Stuttgart 3 -2 katika fainali ya kombe la Shirikisho la Ujerumani mjini Berlin

https://p.dw.com/p/18iRk
Bayern Munich's Philipp Lahm (C) holds up the trophy as he celebrates with his team mates after winning the German soccer cup (DFB Pokal) final match against VfB Stuttgart at the Olympic Stadium in Berlin June 1, 2013. Bayern Munich completed the treble by beating VfB Stuttgart 3-2 in the German Cup final on Saturday, adding the trophy to the Champions League and Bundesliga titles they have already won this season. REUTERS/Fabrizio Bensch (GERMANY - Tags: SPORT SOCCER) DFB RULES PROHIBIT USE IN MMS SERVICES VIA HANDHELD DEVICES UNTIL TWO HOURS AFTER A MATCH AND ANY USAGE ON INTERNET OR ONLINE MEDIA SIMULATING VIDEO FOOTAGE DURING THE MATCH.
DFB Pokal Bayern München gegen VfB StuttgartPicha: Reuters

Goli lake Thomas Müller na mawili kutoka kwa Mario Gomez yaliwapa mabingwa hao wa Bundesliga ushindi wao wa 16 wa kombe la shirikisho, wiki moja baada ya kuwazidi nguvu mahasimu wao wa Borussia Dortmund mabao mawili kwa moja katika fainali ya Champions League uwanjani Wembley. Martin Harnik aliifungia Stuttgart mabao yote mawili.

Stuttgart walijaribu kushambulia

Stuttgart waliwatoa jasho Bayern lakini hatimaye wakashindwa kuwakabili miamba hao wa kabumbu la Ujerumani.

Martin Harnik alikuwa moto wa kuotea mbali kwa upande wa klabu ya VFB Stuttgart
Martin Harnik alikuwa moto wa kuotea mbali kwa upande wa klabu ya VFB StuttgartPicha: Reuters

Wachezaji wa Bayern waliweza kumnyanyua hewani kocha wao Jupp Heynckes, na kumwagia pombe kwa mara ya mwisho.

Kocha wa Stuttgart Bruno Labbadia amesema wamesikitishwa sana na matokeo hayo kwa sababu nafasi ya pili katika kinyang'anyiro hicho kila mara huwa ni upuzi. Lakini wanastahili kukubali kwamba Bayern walipata ushindi kwa sababu ya umahiri wa wachezaji binafsi. Jana ilikuwa mechi ya mwisho kwa Jupp Heynckes kama kocha wa Bayern na sasa anamwachia mikoba Pep Guardiola.

Sasa Bayern ndiyo klabu ya saba barani Ulaya kuwahi kushinda taji la ligi ya nyumbani na kombe la shirikisho na kisha Ligi ya Mabingwa Ulaya au wakati likifahamika kama kombe la Ulaya katika msimu mmoja. Inter Milan (2009/10), Barcelona (2008/9), Manchester United (1998/9), PSV Eindhoven (1987/8), Ajax Amsterdam (1971/2) na Glasgow Celtic (1966/67) ni timu nyingine zilizomo katika kundi hilo maarufu la soka ulimwenguni.

Jupp Heynckes akisheherekea na timu yake baada ya ushindi dhidi ya VfB Stuttgart mjini Berlin
Jupp Heynckes akisheherekea na timu yake baada ya ushindi dhidi ya VfB Stuttgart mjini BerlinPicha: Reuters

Heynckes aaiga Bayern

Heynckes mwenye umri wa miaka 68 amesema atafichua mipango yake ya siku za usoni Jumanne wiki ijayo. Mwenyekiti wa Bayern Karl-Heinz Rummenige tayari amemwambia Heynckes kuwa anaweza kuchagua jukumu jingine analotaka katika klabu hiyo baada ya kushinda taji la Bundesliga na pengo la pointi 25 ambalo halijawahi kushuhudiwa katikahistoria ya kabumbu la Bundesliga.

Kocha huyo anayeondoka anasema yeye ni mzee sana na hawezi kuwa kocha wa klabu nyingine ya ng'ambo na anasisitiza kuwa hana hamu ya kuifunga timu nyingine ya Ujerumani kama siyo Bayern.

Kocha huyo amehusishwa na kurejea katikaklabu ya Real Madrid, ambao aliwaongoza kushinda tajila Champions League mwaka wa 1998. Akizungumzia ushindi wa mataji matatu msimu huu, Heynckes amesema hiyo ni zawadi kubwa ambayo amepewa na timu yake. Nahodha wake Philip Lahm amejigamba kuwa sasa wametimiza kitu ambacho hakijawahi kufanyika katika historia ya soka la Ujerumani.

Mwandishi: Bruce Amani/DPA

Mhariri: Sekione Kitojo