BEIJING : Korea Kaskazini yagoma kuachana na mpango wake wa nuklea
16 Septemba 2005Matangazo
Korea Kaskazini imekataa kuachana na mpango wake wa nuklea iwapo haitopatiwa mtambo mwepesi wa nuklea wa kuzalisha umeme kwa nguvu za maji.
Afisa wa serikali ya Pyongayang amesema mjini Beijing kwamba mtambo huo utakuwa ishara ya kuaminiana kati ya Marekani na Korea Kaskazini.Marekani hadi sasa inapinga kuisaidia Korea Kaskazini kujenga mtambo wa aina hiyo hata kama ni kwa ajili ya dhamira za amani.Korea Kaskazini inasema itakubali ukaguzi na usimamizi wa pamoja wa mtambo huo.
China imesema kwamba mazungumzo ya nchi sita juu ya mpango wa nuklea wa Korea Kaskazini yataweza kuvunjika iwapo pande hizo hazitotia saini taarifa ya pamoja ifikapo hapo kesho.