BEIJING: Marekani na Korea Kaskazini zafanya mazungumzo
19 Desemba 2006Matangazo
Marekani na Korea Kaskazini zimefanya mazungumzo ya ana kwa ana kwa mara ya kwanza kuhusu vikwazo vya kifedha vilivyowekwa na Marekani dhidi ya serikali ya Pyongyang.
Kutengwa kwa Korea Kaskazini mbali na mfumo wa benki wa kimataifa imekuwa sababu kubwa ya nchi hiyo kususia mazungumzo kuhusu mpango wake wa nyuklia kwa zaidi ya mwaka mmoja.
Mazungumzo baina ya Marekani na Korea Kaskazini yamefanyika kandoni mwa mkutano wa mataifa sita kuhusu mpango wa nyuklia wa Korea Kaskazini unaoendelea mjini Beijing China.
Mazungumzo ya leo yalituwama juu ya utekelzwaji wa ahadi za kusalimisha silaha za nyuklia zilizosainiwa na Korea Kaskazini mwaka jana.