BEIJING: Mazungumzo kuhusu mpango wa nuklia wa Korea Kazkazini yaendelea
1 Agosti 2005Matangazo
Wajumbe katika mkutano wa mataifa sita juu ya mpango wa nuklia wa Korea Kazkazini, wamejadili azimio la makubaliano linalotaka Korea Kazkazini ipokonywe silaha za nuklia. Hata hivyo wajumbe wameelezea wasiwasi wao wa kutopatikana makubaliano kamili kufuatia mazungumzo ya wiki moja ya mataifa hayo sita.
Mazungumzo ya sasa hayakuwekewa tarehe ya kumalizuika na yataendelea mpaka makubalianao yatakayoweza kuidhinishwa na pande zote yapatikane.