1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BEIJING: Mazungumzo ya mpango wa nuklia wa Korea Kazkazini yaahirishwa

8 Agosti 2005
https://p.dw.com/p/CEmu

Korea kazkazini na Marekani zimelaumiana kufuatia majuma mawili ya mazungumzo kuhusiana na mpango wa nuklia wa Korea Kazkazini yaliyokwama. Kila upande unaulaumu mwingine kuhusu swala la kuutumia mpango wa nuklia kwa amani, ikiwa makubaliano yoyote yataafikiwa.

Lakini mataifa hayo mawili yanasema upo uwezekano wa kuyafikia makubaliano na yameahidi kuendelea kuwasiliana wakati wa kipindi cha majuma matatu ya mapumziko, kilichotangazwa hapo jana.

Mjumbe mkuu wa China, Wu Dawei, aliwaambia waandishi habari kwamba mapumziko hayo yanalenga kuwapa nafasi wajumbe kuripoti kwa serikali zao kuhusu mkutano huo na kuzimaliza tofauti zilizojitokeza katika mazungumzo hayo.

Wajumbe wa mataifa sita yakiwemo Korea Kazkazini, Korea Kusini, China, Japan, Russia na Marekani, wanatarajiwa kukutana tena mjini Beijing wiki ya mwisho ya mwezi huu.