1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BEIJING: Ujumbe usiokua rasmi wa Marekani kuitembelea Korea ya kaskazini

6 Januari 2004
https://p.dw.com/p/CFld
Habari kutoka mji mkuu wa China Bejing, zinasema ujumbe usiokuwa rasmi wa raia wa Marekani, umeondoka leo hii mjini Beijing, ukielekea katika mji mkuu wa Korea ya kaskazini Pyongyang. Habari hizo zinasema wamarekani hao, wanatarajiwa kutembelea mitambo ya kinuklia ya Yongbyon, ambapo serikali ya Marekani inadai panatengenezewa silaha za kuhilikisha uma. Kiongozi wa ujumbe huo, Bwana John Wilson Lewis, ambae ni mualimu katika chuo kikuu cha Stanford Marekani, alinukuliwa na vyombo vya habari akisema, kwamba kwa sasa yeye na wanzie hawajui ratiba ya ziara yao nchini Korea ya kaskazini, na kwamba watu hawana budi kusubiri hadi watakaporea kutoka Pyongyang.
Wajumbe wengine wanaoandamana nae ni pamoja na mjumbe wa zamani wa serikali ya Marekani nchini Korea ya kaskazini Charles Prichard, pamoja na Bwana Sig Hecker, Mkurugenzi wa zamani wa maabara ya kitaifa mjini Los Alamos. Inasemekana wakuu wa Korea ya kaskazini wamekubali wanaweza kusitisha kwa muda shughuli za vituo vyake vya kinuklia, ikiwa Marekani itaonyesha nia ya kutilia maanani masharti yaliyopendekezwa na Korea ya kaskazini, ili kumalizia kwa njia ya majadiliano, tofauti zilizopo baina ya pande mbili.