1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BEIJING:Mazungumzo juu ya korea kaskazini yaendelea leo

20 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CChv

Wajumbe wa Marekani na Korea Kaskazini kwenye mazungumzo juu ya mpango wa kinklia wa Korea kaskazini wanakutana kwa siku ya pili leo kwa mazungumzo ya ana kwa ana.

Mjumbe wa Mreakani Christopher Hill anatarajiwa kukutana na mwenzake wa Korea kaskazini Kim Kye Gwan mapema leo kabla ya kuanza kikao kingine cha mazungumzo hayo kinachowajumuisha wajumbe wa nchi sita wanaojadili juu ya kuifanya Korea kaskazini iachane na mpango wake wa Kinuklia.

Hapo jana wajumbe hao wawili walishindwa kufikia makubaliano juu ya suala hilo walipokutana kwa mara ya kwanza ana kwa ana.