BEIJING:Mazungumzo ya mataifa sita kuhusu mpango wa nuklia wa Korea Kazkazini yanakaribia kufaulu
1 Agosti 2005Matangazo
Wajumbe katika mkutano wa mataifa sita juu ya mpango wa nuklia wa Korea Kazkazini, wamesema kwamba China imetoa azimio jipya la taarifa ya pamoja.
Taarifa hiyo itakuwa ya kwanza kutolewa kufuatia mazungumzo kama hayo. Maofisa wa Marekani na Korea Kusini wamesema swala nyeti katika azimio hilo ni juhudi zitakazofanywa na serikali nyengine ili Korea Kazkazini ikomeshe mpango wake wa nuklia.
Mazungumzo hayo ambayo yameingia siku yake ya saba leo, yanaonyesha ishara ya kufanikiwa, yakilinganishwa na mikutano mingine, huku kukiwa na mazungumzo ya ana kwa ana kati ya serikali ya Washington na serikali ya Pyongyang.