1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BEIJING:Suala la mpango wa Nuklia wa Korea kaskazini kujadiliwa

18 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CCiZ

Mazungumzo ya pande sita juu ya kuishawishi Korea Kaskazini iachane na mpango wake wa kinyuklia yanaanza leo miezi miwili baada ya taifa hilo kufanya majaribio ya silaha zake za kinuklia.

Wajumbe kutoka nchi za China korea zote mbili Kusini na Kaskazini,Marekani,Japan na Urussi wataanza mazungumzo hayo hivi punde huko Beijing China.

Mjumbe mkuu wa Marekani kwenye mazungumzo hayo Christopher Hill ameitaka Korea kaskazini kutilia uzito suala la kukomesha mpango wake wa kinuklia.

Hill amesema amejiandaa kukutana ana kwa ana na mwenzake wa Korea kaskazini Kim Kye-Gwan ambaye jumamosi iliyopita alikashifu kikao cha leo na kuzishutumu sera za Marekani.

Wajumbe wanaokutana katika mazungumzo hayo watajadiliana jinsi ya kutekeleza makubaliano yaliyofikiwa septemba mwaka 2005 ambapo Korea kaskazini iliahidi kuachana na mpango wake wa kinuklia na kuhakikishiwa usalama pamoja na kupewa usaidizi wa nishati na mahitaji mengine.