Bejing: Tarehe ya mazungumzo ya mpango wa nuklea wa Korea kaskazini yajadiliwa
28 Novemba 2006Matangazo
Wajumbe wa ngazi ya juu wa Korea kaskazini, Uchina na Marekani wamekutana mjini Bejingi kujadili lini yaanze tena mazungumzo ya pande sita, kuhusu mpango wa nuklea wa Korea kaskazini. Mwenyeji Uchina imesema bado hakuna tarehe iliopangwa. Hata hivyo mjumbe wa Korea kaskazini ,Kim Kye-Gwan alisema nchi yake iko tayari wakati wowote. Korea kaskazini ilifanya jaribio la kombora la kinulea mwezi Oktoba lililolaumiwa vikali na jumuiya ya kimataifa, na pia kusababisha vikwazo vya Umoja wa mataifa dhidi ya nchi hiyo