1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bemba hataki kurudi DRC

11 Juni 2007

Muda aliopewa kiongozi wa upinzani Jean Pierre BEMBA wa siku sitini kwa ajili ya matibabu nchini Ureno umemalizika leo lakini Bemba hana mpango wowote wakurejea nchini mwake.

https://p.dw.com/p/CHCs
Jean-Pierre Bemba
Jean-Pierre BembaPicha: AP Photo

Ikiwa atazidisha muda huo Bemba anaweza kupoteza kiti chake cha seneta kulingana na taratibu za ndani za baraza hilo. Itakumbukwa kwamba serikali ya nchi hiyo ilipendekeza kuwa Jean Pierre Bemba afunguliwe kesi ya ughaini kufuatia machafuko ya mjini kinshasa ya mwezi machi,kama anavyoripoti mwandishi wetu Saleh Mwanamilongo.